Mahakama Kuu yawapa haki wafungwa kupiga kura

0
25

Mahakama Kuu nchini imetamka kuwa wafungwa wa makosa ya kawaida ya jinai wana haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu baada ya kubatilisha kifungu cha 11(1) (c) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachoweka zuio kwa wafungwa wanaotumikia adhabu ya kunyongwa na wanaotumikia adhabu ya kifungo cha kuanzia miezi Sita.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Elinaza Luvanda leo Desemba 22 imetokana na shauri la kikatiba lililofunguliwa na raia wawili, Tito Magoti na John Tulla ambao walikosa haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutokana na kuwa mahabusu.

Magoti na Tulla walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu mwaka huu dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Jeshi la Magereza wakidai kuwa kifungu hicho kinakinzana na katiba ibara ya 5(1) ambayo inaeleza kuwa kila raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 anayo haki ya kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Walinzi watatu wauawa wakiwa lindo

Ingawa wadaiwa wakati wa usikilizwaji walipinga madai hayo, walidai kuwa NEC imekuwa ikiwawezesha raia wote kutekeleza haki hiyo kwa mujibu wa sheria, lakini Jaji Luvanda katika uamuzi wake amekubaliana na hoja kuwa kifungu hicho ambacho huweka zuio hilo kwa wafungwa wote wanaotumikia adhabu kuanzia miezi sita, kinakiuka ibara ya 5(1) ya katiba ya nchi.

Amefafanua kuwa Bunge lingeweza kuorodhesha makosa makubwa ya jina ambayo mtu akitiwa hatiani anaondolewa haki hiyo kama vile makosa ya uhaini na mauaji ambayo adhabu yake ni kunyongwa.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend