Mahakama yabariki kuuawa aliyeua mtoto kisa alimrushia mawe

0
88

Mahakama ya Rufani imebariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa Charles Zewanga, mkazi wa Insani wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe kwa kumuua mtoto Lazaro Kayange (10), aliyedai yeye na wenzake walimrushia mawe wakati anaoga mtoni

Wakili wake, Isaya Mwanri aliibua hoja kuwa Jaji aliyemhukumu adhabu ya kifo, hakuzingatia kuwa mteja wake hakuwa na akili timamu na hata wakati kesi ikisikilizwa, alionyesha tabia za kuwa hakuwa timamu ikiwemo kusema kuwa yeye ni mpagani atatoa ushahidi bila kiapo, hivyo akaiomba mahakama ya Rufani ifute adhabu aliyopewa, na kuamuru achunguzwe akili kwanza.

Hata hivyo wakili Mkuu wa Serikali, Revina Tibilengwa amepinga hoja hiyo akieleza kuwa hakuna ushahidi wa kitabibu kuthibitisha hoja hiyo na kwamba alifuatilia mwenendo wa kesi hadi kutiwa hatiani na hakuwahi kuibua hoja ya ukichaa.

Tukio hilo lilitokea Januari 23, 2015 wakati marehemu alipokuwa na watoto wenzake wakichunga ng’ombe pembeni mwa mto Harungwe, na ndipo mshatakiwa alitokea msituni akiwa na mawe na panga na kuanza kuwafukuza, kisha kumshambulia Lazaro huku watoto hao wakishuhudia umbali wa mita 100.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend