Mahakama yafuta kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom

0
65

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imefuta kesi iliyofunguliwa na mwanahabari Erick Kabendera dhidi ya kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania baada ya mahakama kusikiliza pingamizi la awali lililowekwa na Vodacom.

Katika kesi hiyo ya madai namba 12799/2024, Kabendera aliyewakilishwa na Wakili Peter Madeleka alikuwa akiituhumu Vodacom kufanikisha kukamatwa kwake akieleza kama ‘kutekwa’ na hatimaye kufunguliwa kesi hiyo ya uhujumu Uchumi mwaka 2019.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ilisababisha madhara makubwa kwake, yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, kisaikolojia, kutokufurahia Maisha na hadhi yake kwenye jamii, ambapo aliwasilisha madai ya fidia ya Dola za Marekani milioni 10 (TZS bilioni 28) kama fidia kwa hasara alizodai kupata kutokana na tukio hilo pamoja na riba kutoka tarehe ya hukumu hadi malipo yatakapokamilika.

Hata hivyo, Vodacom imefanikiwa kupinga kesi hiyo ambapo Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Livin Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kuifuta.