Mahakama yamhukumu miaka 90 kwa ubakaji

0
86

Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka 90 Leonce Athanas Matea maarufu ‘Alaji’ (55), mkazi wa Chicago A’ Kata ya Kidatu wilayani humo, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya ubakaji wa watoto watatu.

Hukumu hiyo imetolewa Mei 27, mwaka huu na Hakimu Bestina Saning’o baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliothibitisha pasi na shaka mashtaka yote matatu dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu Saning’o amesema adhabu zote katika mashtaka yote matatu zitakwenda kwa pamoja, hivyo mshtakiwa atatumikia adhabu ya kifungo hicho kwa kuishi gerezani kwa miaka 30.

Send this to a friend