Mahakama yampa ruhusa kukusanya manii ya mume wake aliyefariki

0
24

Katika tukio la kushangaza, mwanamke mwenye umri wa miaka 62 nchini Australia ameruhusiwa kukusanya manii ya marehemu mumewe, akiwashawishi majaji kuwa wawili hao walipanga kuwa na mtoto kabla ya kifo chake.

Wawili hao walianza kufikiria kuwa na mtoto mwingine baada ya mtoto wao mwenye umri wa miaka 31 kufariki kwenye ajali ya gari mnamo 2019, na miaka sita baadaye walimpoteza binti yao mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuzama majini kulingana na nyaraka za kisheria zilizotolewa Jumatano.

Kufuatia msururu wa matukio hayo ya kuhuzunisha, wapenzi hao walianza kufikiria ikiwa manii ya mume wake mwenye umri wa miaka 61 yanaweza kutumika kumpa ujauzito mwanamke wa ziada, na baada ya kifo cha mumewe mnamo Desemba 17, mkewe aliomba hospitali ikusanye na kuhifadhi manii yake.

Hata hivyo, hospitali ilisita kutoa huduma hiyo na mwanamke huyo kulazimika kutafuta amri ya Mahakama Kuu nchini Australia ambapo ombi la mwanamke huyo likikubaliwa kwa kufuata mchakato uliotolewa na mahakama.

Ingawa si jambo la kawaida, si mara ya kwanza kwa manii kukusanywa kutoka kwa wapenzi waliofariki nchini Australia. Mnamo Juni 2023, mwanamke mmoja alipewa ruhusa ya kukusanya manii kutoka kwa mumewe mwenye umri wa miaka 29 ambaye alifariki.

Watafiti wanasema tishu za uzazi zinapaswa kukusanywa kati ya siku moja na mbili baada ya kifo.

Send this to a friend