Mahakama yamuongezea adhabu Diwani wa ACT Wazalendo aliyekata rufaa

0
52

Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo ameongezewa adhabu ya kifungo jela kutoka miezi mitano hadi mwaka mmoja, baaada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali.

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 10, 2019 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, ambapo kiongozi huyo alikata rufaa kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani (F.8350 PC), Msafiri Mponela.

Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.

Send this to a friend