Mahakama yaruhusu Makonda kushitakiwa kwa makosa ya jinai

0
20

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeruhusu kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mahakama imetoa taarifa hiyo ikijibu maombi ya mwandishi wa habari, Saed Kubenea kufuatia malalamiko aliyowasilisha mahakamani hapo kutokana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kinondoni kumkatalia kufungua mashitaka dhidi ya kiongozi huyo.

Paul Makonda aongezewa mashitaka

Barua hiyo ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Joseph Luambano imeeleza kuwa Kubenea anayo haki ya kufungua shauri la jinai dhidi ya Makonda.

Kubenea ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Ubungo anamtuhumu Makonda kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds Media Group na kuingilia urushaji wa matangazo ya kipindi Machi 17, 2020.

Isome hapa hati ya mashitaka yanayomkabili Paul Makonda

Mbali na Makonda, Kubenea anawashitaki pia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ambao anadai walishindwa kumchukulia hatua Makonda alipotenda makosa hayo.

Makonda: Mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu

Awali, ombi la kufungua kesi hiyo lilikataliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni. Mahakama ya Kisutu pia ilikataa kwa maelezo kwamba ili kufungua kesi ya jinai lazima kuwepo na hati ya mashitaka ya mahakama ya mwanzo, na pili hati ya kiapo haikuonesha namna gani DPP ameshindwa kuchukua hatua za kumshtaki Makonda.

Send this to a friend