Mahakama yasema kuondolewa kwa CAG, Prof. Assad kulikuwa batili

0
43

Mahakama Kuu Tanzania imesema uamuzi wa kumwondoa kwenye utumishi wa umma aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ulikuwa batili.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe imeatolewa uamuzi huo leo Desemba 5, 2022 akidai kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba inaeleza kuwa CAG atatumikia wadhifa huo mpaka umri wake wa kustaafu, yaani miaka 60 kikatiba au miaka 65 kisheria sawa na kifungu 62(a) cha sheria hiyo kinavyoeleza.

Zitto alikuwa akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba na kwamba kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kutimiza umri wa kustaafu ni batili na pia uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya ni batili.

Mahakama imesema kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kulikuwa ni batili huku ikikataa maombi ya Zitto kutamka kuwa uteuzi wa Kichere ni batili, badala yake imesema kuwa uteuzi wake ni halali kwa kuwa aliteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

Profesa Assad aliteuliwa kushika wadhifa huo na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete Novemba 5, 2014 na kuhudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi Novemba 4, 2019 baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kumteua Charles Kichere kushika wadhifa huo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend