Mahakama yashindwa kutoa hukumu kwa Aveva na Kaburu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mkoani Dar es Salaam imeshindwa kutoa hukumu katika inayomkabili aliyekuwa Rais wa Simba SC, Evansi Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu.’
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema hajamaliza kuandika hukumu ya shauri hilo, hivyo amesogeza mbele tarehe ya kutoa hukumu hadi Oktoba 21 mwaka huu.
Mahakama hiyo iliwakuta washtakiwa Aveva, Kaburu na Hans Pope na kesi ya kujibu katika mashitaka manne ikiwemo kosa kula njama, kughushi nyaraka, na kutoa maelezo ya uongo.
Katika kesi ya msingine watuhumiwa hao walikutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka manne likiwemo la kula njama, kughushi nyaraka na kutoa maelezo ya uongo.