Mahakama yatengua hukumu ya Mfalme Zumaridi

0
56

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetengua hukumu ya kifungo cha miezi 12 aliyopewa Diana Bundala (Mfalme Zumaridi) na wenzake nane baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzuia maofisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao.

Katika kesi hiyo ya rufaa, upande wa mjibu maombi ulikata rufaa kupinga adhabu hiyo kuwa ndogo kwa mujibu wa sheria, huku upande wa Zumaridi ukikata rufaa kupinga adhabu hiyo ukidai haikustahili kutolewa.

Akitoa uamuzi huo Jaji Dkt. Cleoface Morris amesema baada ya kupitia vielelezo na maelezo ya mashahidi yaliyotumika kuwatia hatiani waleta maombi katika kesi ya jinai namba 10/2023, Jamhuri ilishindwa kuthibitisha kuwa waleta maombi walitenda kitendo kiovu na walikuwa na nia ovu kwa maofisa wa Serikali ambao wanadai kushambuliwa nyumbani kwa mhubiri huyo.

JWTZ yatoa siku saba wenye sare za jeshi au nguo zinazofanania kuzisalimisha

“Kwenye maelezo na vielelezo vilieleza kwamba maofisa wa Polisi, Wakili wa Serikali na Ofisa Ustawi wa Jamii walifika katika makazi ya mleta maombi namba moja (Zumaridi) wakati wakitambua kuwa mbali na kuwa makazi, pia ni eneo la ibada hivyo kwenye ushahidi hawakuthibitisha iwapo walienda kufanya kitu gani, kwa ajili ya nani na kwa nini,” ameeleza.

Ameongeza, “Kuna uwezekano watenda wa kitendo kile walidhani kuwa maofisa hao wa Serikali ni waumini hivyo kitendo cha kujaribu kufanya kinyume na shughuli zinazotendeka pale bila kuweka bayana kilichowapeleka haikuwa sahihi.”

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend