Mahakama yatengua zuio lililowekwa dhidi ya wasiochanjwa

0
43

Mahakama ya juu nchini Kenya imesitisha agizo la serikali linalotaka kuwazuwia watu ambao hawajapata chanjo kutoruhusiwa kuingia na kupata huduma kwatik ofisi za umma.

Hoja iliyowasilishwa na mfanyabiashara Enock Aura imeeleza kuwa mwongozo huo ambao ulitarajiwa kutekelezwa wiki ijayo, ni kinyume cha katiba na ni wa ubaguzi.

Mahakama imesema zuio hilo halitotekelezwa hadi hapo kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na mahakama.

Akitangaza uamuzi huo mapema Novemba mwaka huu Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe alisema kuwa agizo hilo linalenga kuwawezesha Wakenya zaidi kupata chanjo.

Serikali imepanga kuwachanja Wakenya milioni 10 kufikia mwisho wa mwaka huu ambapo hadi sasa watu milioni 8.1 tayari wamepata chanjo ya UVIKO19.

Kuahirishwa kwa agizo hili pia kunakuja siku kadhaa baada ya hoteli na maduka makubwa kadhaa kutangaza kuwa hayatawaruhusu Wakenya ambao hawajapokea chanjo kuingia kwenye mazingira yao.

Send this to a friend