Mahakama yatoa hukumu kesi ha Maxence Melo na Mike Mushi

0
54

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtia hatiani Mkurugenzi wa Jamiiforums Maxence Melo, katika shitaka namba mbili la kuzuia upelelezi wa jeshi la polisi.

Katika huku iliyotolewa leo mahakamani hapo, Melo ameachiwa kwa sharti ya kutokufanya kosa kama hilo ndani ya mwaka mmoja.

Katika shtaka hilo, Melo na Mike Mushi walishtakiwa kwa kukataa kutoa taarifa za wanachama wawili waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea CRDB, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mamlaka ya bandari.

Taarifa za wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni
IP-address, barua pepe, majina yao halisi. Pia machapisho yao yote yanayohusu uhalifu huo yalitakiwa kitolewa.

Aidha, katika shitaka la kwanza la kutosajili Jamiiforums kwa kikoa cha Dot-TZ (.tz) Melo hajakutwa na hatia.

Mshitakiwa namba mbili katika kesi hiyo namba 458 ya mwaka 2016 hajakutwa na hatia katika tuhuma zote kwenye kesi hiyo.

Send this to a friend