Mahakama yatoa msimamo wa Tanzania kuhusu adhabu ya kifo

0
53

Mahakama Kuu ya Tanzania imesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa adhabu ya kifo inakiuka katiba ya nchi.

Watetezi wa haki za binadamu walifungua kesi mahakamani wakitaka adhabu hiyo iondolewa kwa maelezo kuwa inakiuka haki ya msingi ya kuishi ya wananchi, ambayo katiba imeitoa.

Kutokana na uamuzi huo wa mahakama, adhabu hiyo itaendelea kuwapo nchini.

Licha ya adhabu hiyo kuwepo nchini, kwa miaka 25 sasa adhabu hiyo haijatekelezwa huku wafungwa takribani 500 wanasubiria adhabu hiyo, au wengine wamebadilishiwa adhabu hiyo na kupewa kifungo cha maisha jela.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 18 barani Afrika ambazo zina adhabu hiyo, lakini hazijaitekeleza kwa kipindi cha muongo mmoja (miaka 10) uliopita.

Nchi 15 za Afrika zikiwemo Botswana, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan, Sudan Kusini na Ethiopia zimekuwa zikitekeleza sheria hiyo.

Hapa chini ni ramani ya Afrika ikitoa maelezo kuhusu sheria ya adhabu ya kifo Afrika:

Send this to a friend