Mahakama yatupilia mbali maombi ya Lissu ya kupinga mashahidi wa siri

0
103

Mahakama Kuu Masijala Ndogo, Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kupinga mashahidi wa siri katika kesi inayomkabili ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni.

Lissu alipinga maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam kuhusu mashahidi ambao si askari kufichwa utambulisho wao katika kesi hiyo na badala yake alitaka mashahidi waonekane ili waweze kuhojiwa mahakamani.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema kama chama wamepanga kushauriana ikiwa watakata rufaa kupinga maamuzi hayo au la.

Send this to a friend