Mahakama yatupilia mbali kesi ya Mdee na wenzake 18

0
49

Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Maamuzi hayo yamefikiwa hii leo baada ya wanachama hao 19 wakiongozwa na Halima Mdee kupinga kuvuliwa uanachama wao na Baraza Kuu la CHADEMA.

Mdee na wenzake waliomba ruhusa ya Mahakama ili iweze kufungua shauri la kupitia upya uamuzi wa CHADEMA uliofanywa Mei 11, mwaka huu kuhusu kufukuzwa uanachama wao.

Mara baada ya kufungua shauri hilo, walifungua shauri dogo la maombi namba 13 la mwaka 2022, wakiomba zuio la muda dhidi ya NEC na AG kubatilisha nafasi zao kama wabunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Send this to a friend