Mahakama yatupitilia mbali pingamizi la Sabaya na wenzake

0
42

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.

Mawakili wa Sabaya na wenzake watano waliweka pingamizi la awali jana Desemba 13, 2022 katika kesi ya rufaa waliyofunguliwa na na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Salma Maghimbi leo Jumatano Desemba 14, 2022 ambaye anasikiliza shauri hilo baada ya jana kusikiliza hoja za pande zote mbili.

Send this to a friend