Mahakama yaulinda ubunge wa Mdee na wenzake

0
62

Mahakama Kuu Kanda ya Dar esa Salaam imetoa zuio la muda kuhusu kutofanyika chochote kwenye ubunge wa Halima Mdee na wenzake 18 mpaka pale itakaposikiliza maombi ya rufaa yao.

Zuio hilo limetolewa leo Juni 27 baada ya kesi ya wabunge hao kurudishwa mahakama kuu baada ya marekebisho yaliyopelekea kutupiliwa mbali maombi yao Juni 22, mwaka huu.

Hata hivyo, kwa sasa maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo yanalenga kulishtaki Baraza la Wadhamini badala ya Bodi ya Wadhamini iliyokuwa ikishtakiwa hapo awali.

Mdee na wenzake walivuliwa uanachama na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kamati kuu ya chama hicho.

Send this to a friend