Mahakama yavunja ndoa ya Kafulila na Jesca, suala la watoto laamuliwa

0
47

Ndoa ya wanasiasa machachari, David Kafulila na Jesca Kishoa imevunjwa rasmi na Kituo Jumuishi Huduma za Kimahakama, Mirithi na Ndoa baada ya ndoa hiyo kushindwa kurekebishika kwa madai ya ugomvi na utengano wa wanandoa hao.

Ndoa hiyo iliyofungwa Aprili 22, 2014 imevunjwa rasmi Februari 20, 2023 baada ya wanandoa hao kutengana tangu mwaka 2019 na mahakama kujidhihirisha kuwa ndoa hiyo haiwezi kurekebishika.

Mahakama imevunja ndoa baina ya wawili hao huku ikitoa amri kwa mama kubaki na watoto na kila mzazi kuwa na wajibu wa kuchangia gharama za matunzo kwa asilimia 50.

Jeshi la Polisi: Tumeona video za askari, tunafanya uchunguzi pamoja na kumpima

“Kwa msingi huo amri ya kuivunja ndoa na talaka inatolewa. Sambamba na hilo, watoto wataishi chini ya uangalizi wa mama yao. Mjibu maombi atakuwa na haki ya kuwaona na kuwa na watoto wake mwishoni mwa juma na vipindi vya likizo za masomo,” ameeleza Hakimu Swai.

Aidha, katika hukumu hiyo ameeleza kuwa chini ya kifungu 129 cha Sheria ya Ndoa, mjibu maombi anawajibika kutoa matunzo ya watoto kikamilifu.

Send this to a friend