Maharage Chande: Hakuna mgao wa umeme Tanzania

0
51

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kuwa hakuna mgao wa umeme Tanzania na kwamba changamoto ya kukatika kwa umeme inatokana changamoto za usambazaji wa umeme na sio uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande amesema hayo leo asubuhi akizungumza kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kudadavua kwamba wanaendelea kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha watu wanapata umeme wa uhakika.

“Hatuna tatizo la generation [uzalishaji]. Ukizungumzia mgao ni kwamba una watu wanataka halafu wewe huna wa kuwapa wa kutosha, ndio mgao. Hatuna mgao wa umeme. Tanzania changamoto ya ukatikaji wa umeme ni ku-improve service [boresha huduma] yetu kwenye usambazaji,” ameeleza Chande.

Aidha, amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na matengenezo ya njia za usambazaji na kwamba ndani ya miezi sita tatizo hilo litamalizika. Amesisitiza kuwa TANESCO ina majukumu makuu matatu ambayo ni kuzalisha umeme, kuusafirisha na kuusambaza kwenye makazi ya watu na maeneo mengine.

Send this to a friend