Maharusi watatu wafunga ndoa pamoja kupunguza gharama

0
29

Janga la Virusi vya Corona si tu limeathiri watu kiuchumi, lakini pia kijamii hasa namna watu wanavyoshiriki katika shughuli zinazohusisha idadi kubwa ya watu.

Katika Kijiji cha Kapkiruok nchini Kenya kumefanyika harusi iliyowaacha watu midomo wazi baada ya maharusi watatu kutoka familia tofauti kufunga ndoa pamoja ili kuokoa gharama.

Familia za maharusi hao zimeridhia kufanya sherehe ya pamoja ili watumie fedha kidogo kutokana na janga la corona kuathiri vyanzo vyao vya mapato.

Wanaume hao walisafiri kutoka maeneo mbalimbali, Bungoma, Uasin Gishu na Keiyo kufanikisha sherehe hiyo. Hata hivyo wameeleza kuwa halikuwa jambo rahisi kufikia muafaka.

Wanandoa hao wamewashauri vijana kutumia njia mbalimbali ikiwemo ya ndoa ya pamoja kupunguza gharama za ndoa, jambo ambalo wakati mwingine zinapelekea vijana wengine wasioe.

Wanandoa hao wapya wamesema walitumia muda mrefu kupanga tukio hilo ambapo baadhi ilibidi waahirishe tarehe zao za kufunga ndoa walizokuwa wamesema awali ili kufanikisha ndoa ya pamoja.

Send this to a friend