Mahesabu ya ubingwa yanaibeba zaidi Simba SC

0
40

Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Alhamisi.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na John Bocco (32), Clatous Chama (47) na Emmanuel Okwi (57), na hivyo kuifanya timu hiyo kutoka kifua mbele ikizidi kutengeneza njia ya kutwaa ubingwa.

Ushindi huo unawapeleka Simba kileleni baada ya kufikisha alama 85, huku Yanga wakivutwa hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 83, huku Mtibwa Sugar iliyokubali kipigo inasalia nafasi ya 5 ikiwa imejikusanyia alama 49.

Kipindi cha kwanza kati ya Simba na Kagera Sugar kilimalizika kwa Simba kuwa mbele kwa bao 1-0, bao lililofungwa dakika 32 na John Bocco ambaye amefikisha jumla ya mabao 15, msimu huu.

Kipindi cha Simba walirejea uwanjani kwa ari kubwa na kwamba licha ya nafasi walizopoteza waliweza kufunga magoli mengine mawili.

Yanga yenye alama 83 ina mechi mbili zimesalia na endapo itashinda zote, itakuwa na alama 89. Lakini kwa upande wa Simba wao wananafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwani mbali na kuwa wanaongoza ligi wakiwa na alama 85, lakini bado wana michezo minne mkononi.

Hii ina maanisha kuwa, Simba akishinda michezo miwili kati ya minne iliyosalia, tayari atakuwa ametwaa ubingwa, kwani atafikisha alama 91 ambazo hakuna timu nyingine inaweza kufikia.

Hata Simba ikitoka sare michezo yote minne, bado ina nafasi kubwa ya kushinda kwani itakuwa sawa na Yanga (kama watashinda) na kuwa na alama 89 wote, lakini Simba ina tofauti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Send this to a friend