Majaliwa aagiza watumishi wanne wa TRA waondolewe kutokana na dharau

0
47

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) cha Mutukula, Feisal Nassoro na wenzake watatu warudishwe makao makuu mara moja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na kudharau mamlaka na kuikosesha Serikali mapato.

Ametoa agizo hilo Septemba 23, 2023 wakati akizungumza na wafanyabiashara na wakazi wa Mutukula mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (One Stop Border Post) cha Mutukula, wilayani Missenyi mkoani Kagera ambapo amesema watumishi hao walidharau Kamati ya Usalama ya Wilaya wakati wa ukaguzi ulioongozwa na mkuu wa wilaya.

“Mkuu wa Wilaya ni mkuu na msimamizi wa shughuli za Serikali ndani ya wilaya yake. Anapotaka taarifa anastahili apatiwe. Uongozi wa mkoa ulipokuja nao pia waliambulia dharau. Hatuwezi kukubali kuona mtumishi wa umma anafanya mambo ya hovyo halafu sisi tunamwacha,” amesisitiza Waziri Mkuu.

ATCL yasitisha safari kwenda China

Watumishi wengine waliochukuliwa hatua ni Gerald Mabula, George Mwakitalu na Emmanuel Malima ambao ni maafisa mapato wa TRA.

Send this to a friend