Majaliwa aahidi kusimamia madai ya madereva na haki za waajiri

0
37

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inaendelea kusimamia madai ya madereva pamoja na haki za waajiri katika kutekeleza madai ya madereva wa malori.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na na viongozi mbalimbali juu ya kuwepo kwa mgogoro wa madereva na waajiri kuhusu maslahi yao.

“Lengo ni kuhakikisha madereva wanaendelea na ajira zao na wanapata maslahi yao kwa mujibu wa sheria ili waweze kuendesha shughuli zao na familia zao na Serikali itasimamia madai yao na haki za waajiri katika kutekeleza madai ya madereva wasije wakawajibika na vitu ambavyo haviko kwenye sheria zetu za nchi,” amesema.

Tangazo la nafasi ya kazi Mfuko wa Utamaduni na Sanaa

Aidha, ametumia fursa hiyo kukitaka Chama Cha Madereva nchini kuruhusu huduma za usafirishaji ziendelee kutolewa wakati Serikali ikiendelea kushughulikia masuala yao na kusema kuwa Serikali haitaridhika kuona madereva wanalalamika kila siku na pia si vizuri waajiri wakabebeshwa mizigo iliyo nje ya sheria.

Majaliwa amesema malalamiko ya madereva hao ni kutopewa mikataba ya kazi, kutokuwa na uhakika wa matibabu yao na familia zao (bima ya afya), kupewa mishahara yao mikononi badala ya benki na kutounganishwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili wawe na uhakika wa kupata mafao baada ya kustaafu.

Send this to a friend