Majaliwa: Acheni kutafuta uongozi kwa kutengeneza fitina na migogoro

0
35

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaonya watu wanaotafuta madaraka kwa kutengeneza fitina na mbinu nyingine chafu za kuharibia wengine kwenye uongozi, na kuwataka wafahamu kwamba uongozi unapangwa na Mungu.

Akizungumza hivi karibuni jimboni kwake Ruangwa mkoani Lindi, Majaliwa alisema kwamba kila kitu kinapangwa na Mungu kwamba nani atakuwa nani katika kipindi gani, hivyo mwanadamu akilazimisha hatofanikiwa kama Mungu hajapanga.

“Usitumie njia yoyote ya kumwathiri mwenzako ili upate madaraka eti atoke hapo wewe uende. Nani amekwambia utakwenda? Nani amezungumza na Mungu? Utatumia mihela mingi itapotea, utakwenda na mambo ya giza, hutakwenda. Mungu amesema huyu ni huyu. Tuheshimu walioko kwenye nafasi ya kuwatumikia Watanzania,” amesema kiongozi huyo.

Amesema jukumu la Watanzania kila mmoja kwa imani yake ni kuwaombea viongozi wawe na busara na kufahamu ni kitu gani Watanzania wanakihitaji. Amesisitiza kwamba hakuna haja ya kutengeneza migogoro kila siku bali viongozi waachwe wafanye majukumu yanayowahusu.

Send this to a friend