Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Arusha

1
89

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima pamoja na baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za unadhirifu wa fedha za Serikali TZS milioni 233 zinazodaiwa kuwekwa kwenye akaunti za watu binafsi.

Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na watumishi wa Jiji la Arusha kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja Jijini Humo.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima alikuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Tabora. Pia alikuwa Mhadhiri katika Chuo Cha Uhasibu Arusha tangu mwaka 2006.

Send this to a friend