Majaliwa amsimamiza kazi afisa manunuzi aliyejipa zabuni

0
35

Waziri Mkuu Kassim amesemamisha kazi Afisa Mipango wa Halamshauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Omary Chinguile kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma ambapo ujenzi huo umetumia fedha nyingi kuliko zilizotakiwa na kuwepo mgongano wa kimaslahi katika ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.

Akizungumza na madiwani pamoja na wananchi akiwa ziarani mkoani humo, Waziri Mkuu ameeleza kushangazwa na taarifa za mwekahazina wa wilaya hiyo kwamba wametumia zaidi ya TZS bilioni 1.8 katika ujenzi wa hopsitali hiyo na ujenzi haujakamilika, huku mkandarasi akisema anataka milioni 300 zaidi kukamilisha ujenzi.

Waziri Mkuu amekerwa mhasibu hiyo kuchukua zaidi ya milioni 500 na kumpa Chingule kwenda kunua vifaa vya ujenzi, wakati ujenzi wenye haukuwa umeanza, na hajui vifaa vya kiasi hicho cha fedha vilihifadhiwa wapi.

Baada ya kunua vifaa hivyo, walichukua fedha za halmashauri ili mradi huo uanze, lakini hawakueleza kama fedha hizo wamekopa ama la, na kama fedha za serikali kuu zikipelekwa, watarudisha fedha za halmashauri.

Kuhusu mgongano wa kimaslahi, Chingule akiwa kama afisa manunuzi alijipa zabuni ya kupepeleka mchanga na kokoto kwa ajili ya ujenzi huo (tripu 48 za mchanga, 8 za kokoto) lakini tangu Julai 2021 amepeleka tripu 48 za mchanga na moja ya kokoto na tayari amejilipa milioni 12. Hata hivyo fedha hizo zilipokelewa na dereva wake, Hassan Kidunga.

“Injinia anasema anataka milioni 300 akamilishe hospitali ya wilaya, huku mna mgao wa shilingili bilioni 1.5, mmechukua hela ya madiwani mmeiweka hapo, manataka tena kuomba milioni 300 kutoka mapato ya ndani, nyiie,” amesema waziri mkuu.

Majaliwa amesema kuwa serikali haitavumilia watendaji wabadhirifu, na ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kumchunguza afisa huyo.

Send this to a friend