Majaliwa ataka wizara ieleze hatima ya waliolipa viingilio Simba vs Yanga

0
37

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka kuhusu lini mchezo wa Simba SC na Yanga SC ulioahirishwa utachezwa na hatima ya waliolipa viingilio.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo leo bungeni mjini Dodoma na kueleza kuwa kuahirishwa kwa mchezo huo wa watani wa jadi kumesababisha sintofahamu kubwa hasa kwa wapenda mpira wa miguu.

Ameiagiza wizara kutoa taarifa hiyo kwa kushirikiana na taasisi inayoendesha mchezo huo nchini ambayo ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mchezo namba 208 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya
Simba na Yanga ulitakiwa kuchezwa Mei 8, 2021 lakini uliahirishwa baada ya kuibuka mkanganyiko uliotokana na mchezo huo kusogezwa mbele kwa saa mbili kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 jooni, taarifa iliyotolewa saa chache kabla ya mchezo kuanza.

Send this to a friend