Majaliwa: Tuwe na subira matokeo yakiendelea kutolewa

0
12

Siku moja baaxa ya Watanzania kupiga kura kuchagua Rais, wabunge na madiwani, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuwa wmna subira wakati matokeo yakiendelea kutolewa.

Ametoa wito huo katika sherehe za Baraza la Maulid, lililofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee.

“Vyama vya siasa, wagombea, wafuasi wa wagombea na kila mdau anayeitaki heri nchi hii, kuwa na utulivu na wenye subira wakati huu matokeo yanaendelea kutolewa,” amesema Majaliwa akiwasihi wananchi kulinda amani.

Amesema kuwa katika kipindi hiki ni muhimu sana kujiepusha na kauli au vitendo ambavyo vinaweza kupandikiza chuki na uhasama dhidi yetu au waumini wa imani nyingine. “Nitoe rai kwenu viongozi wangu na waumini wenzangu tuendelee kuvumiliana na kustahimiliana hususan pale zinapotokea tofauti miongoni mwetu.”

Naye Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisisitiza suala la amani nchini kwani ni kielelezo kikubwa katika kuielezea Tanzania nje ya nchi.

Send this to a friend