Majambazi wasimamisha mahubiri kanisani na kuwaibia waumini

0
58

Majambazi waliokuwa na silaha wamevamia kanisa huko Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuwapora waumini huku wakiwatisha kwa bunduki, Jumamosi Novemba 26 mwaka huu.

Kamera ya kanisa hilo iliwanasa majambazi hao ambao walisimamisha ibada na kuanza kukusanya pesa na vitu vya thamani kutoka kwa watu waliohudhuria ibada katika kanisa la SDA la Johannesburg Central,

Viongozi wa kanisa hilo baadaye walituma ujumbe wa kuwafariji waumini wao na kuwataka kuhudhuria ibada ya ushauri siku ya Jumapili, siku moja baada ya tukio hilo.

Polisi walaumu panya kwa kula 200kg za bangi za ushahidi

”Kanisa linapenda kuchukua nafasi hii kuwahakikishia kuwa hili nalo litapita. Hakuna kinachodumu milele. Kama viongozi, tunaombea kanisa kuungana katika nyakati kama hizi tukisaidiana kimaadili na kimatendo,” umesema ujumbe huo.

Send this to a friend