Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kuanza majaribio ya kutoa huduma katika Reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro Februari, mwaka huu.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amebainisha kuwa kazi ya ujenzi wa reli ya kisasa awamu ya kwanza kilomita 1,219 kati ya Dar es Salaam na Mwanza na kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro kilometa 300 kilimefikia asilimia 99.77.
“Awamu hii ya kwanza pekee inatarajiwa kugharimu TZS trilioni 16 na kati ya fedha hizo tayari Serikali imeshatoa kuwalipa wakandarasi kiasi cha TZS trilioni 8.143,” amesema.
Nauli mpya za mwendokasi zitakazoanza kutumika Januari 16, 2023
Aidha, Msigwa amesema awamu ya pili itahusisha kipande cha Tabora – Kigoma, kilometa 506 zinazojumuisha njia kuu za kilometa 411 na mapishano kilometa 95 na tayari mkataba wa ujenzi umesainiwa na wakandarasi wapo eneo la tukio.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa mabehewa 14 mapya yaliyotengenezwa Korea Kusini tayari yamewasili nchini na yanasubiriwa mabehewa 45 huku vichwa 17 vya treni za umeme na seti za treni vikiendelea kutengenezwa.