Majibu 8 kuhusu programu mpya ya ‘Threads’ inayoshindana na Twitter
‘Threads’ ndiyo programu inayoongelewa zaidi kwa sasa kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Meta, Mark Zuckerberg na kuzusha mjadala mkubwa ikiwa programu hiyo inayolenga kuipindua programu ya Twitter itafanikiwa kama ilivyopanga?
Ikiwa unataka kufahamu aina hii ya programu, malengo yake na namna inavyofanya kazi, fuatilia makala hii kujua zaidi;
1.Threads ni nini na inafanyaje kazi?
Threads ni programu iliyounganishwa na Instagram ambayo inaonekana kama mbadala wa Twitter. Kama ilivyo kwa Twitter, inaruhusu watumiaji kuandika na kushirikishana machapisho yao ambayo watu wanaweza ‘ku-like’ na kujibu (reply) pamoja na kushirikisha wafuasi wao.
2.Ni wapi watumiaji wanaweza kuipata Threads ?
Meta imesema inalenga kusambaza Threads katika zaidi ya nchi 100. Umoja wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya haukujumuishwa kwa sababu ya sheria zilizopo.
3.Watumiaji wanawezaje kupakua programu ya Threads?
Ili kujiunga na Threads, watumiaji wanahitaji akaunti ya Instagram na iPhone au kifaa cha Android. Programu hiyo inapatikana kwenye ‘App Store’ kwa iPhones na Google Play Store kwa vifaa vya Android.
4.Je, watumiaji wa Twitter wanaweza kuhamisha wafuasi wao hadi kwenye Threads?
Hapana. Kila mfuasi atahitaji kuwatafuta kwenye Threads, na hiyo ndiyo sababu moja kwa nini ni vigumu kwa Meta kuvuruga biashara iliyoanzishwa kama Twitter. Watu mashuhuri wa Twitter ambao wametumia miaka mingi kujenga wasifu wao wanaweza kufikiria mara mbili kabla kutafuta wafuasi wapya kwenye Threads.
5.Je, Threads imeunganishwaje na Instagram?
Kwa sasa haiwezekani kufuta akaunti yako ya Threads bila pia kufuta akaunti yako ya Instagram, na ukizuia akaunti kwenye Threads, pia imezuiwa kwenye Instagram. Watumiaji wa Instagram wanaojiunga kwenye Threads hupewa beji ya Threads kwenye ukurasa wa akaunti yao ya Instagram ambayo inaonesha namba ya kujiunga.
6.Kwa nini Meta inazindua mbadala wa Twitter?
Meta iko wazi kuhusu kutaka kuwinda watumiaji wa Twitter. Zuckerberg alisema kunapaswa kuwa na programu ya mazungumzo yenye watu bilioni 1 na zaidi, na kwamba Twitter haijaweza kuthibitisha hilo.
7.Ni watu wangapi wamekuwa wakiondoka Twitter?
Watu kadhaa mashuhuri walio na wafuasi wengi waliacha kuitumia muda mfupi baada ya Musk kuchukua wadhifa huo, akiwemo nyota wa televisheni Oprah Winfrey na mwanamuziki Elton John, ambao akaunti zao hazituma ujumbe wowote tangu mwisho wa 2022.
8.Je, ni kweli Threads imekuja kuisambaratisha Twitter?
Baadhi ya wachambuzi wanafikiri kuwa ni jambo linalowezekana kuwa Meta inaweza kukamata sehemu kubwa ya twitter ambao ni watumiaji na matangazo, haswa ikiwa uzinduzi wa Threads kutaambatana na ahadi ya Meta kwamba kutakuwa na juhudi za kupunguza usambazaji wa habari potofu.
Wengine wana shaka na wanaona chapa ya Meta kama isiyo rasmi zaidi kuliko Twitter, ikipunguza mvuto wake kwa aina fulani za watumiaji.