Majibu ya UDOM kwa wanaohoji PhD za mawaziri Doto Biteko na Selemani Jafo

0
40

Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM) kimesema kwamba wenye mashaka juu Shahada za Uzamivu (PhD) zilizotunukiwa kwa viongozi wa kisiasa hasa mawaziri na wabunge wanaweza kutembelea maktaba ya chuo hicho kuona machapisho ya wahitimu husika.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Faustine Bee akizungumza na gazeti la Mwananchi na kueleza kwamba suala la viongozi hao kuhitimu PhD inategemea na wanavyojipanga, kupangilia muda kazi na masomo yake kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya chuo na wasimamizi.

“Mimi sioni shida mtu kuhitimu kama anazingatia hayo,” amesema Prof. Bee akiongeza kwamba si sahihi kumhukumu mtu kwa sababu ni mwanasiasa kwani wapo wengi wanaosoma na kuhitimu ingali bado wapo kazini.

Amesema mawaziri na wabunge hao wamefuata utaratibu wa usimamizi na kuwasilisha mawasiliano ambayo waliyatetea mbele ya jopo la wanataaluma.

Mjadala huo uliibuliwa na mwanazuioni Prof. Mark Mwandosya aliyehoji kama viongozi kwenye nafasi hizo wanauwezo wa kutimiza majukumu yao na kunandika tasnifu na mahitaji mengine hadi kufikia kuhitimu PhD, au vigezo vimebadilika.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Waziri katika Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ambaye ni miongoni mwa wahitimu  42 waliotunikiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Desemba 16, 2021.

Send this to a friend