Spika wa Bunge la Tanzania, Job Nduga ameagiza Kitengo cha Usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge 15 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuingia katika maeneo ya Bunge kuanzia leo Mei 13, 2020.
Kwa kujibu wa taarifa ya Ofisi ya Spika wa Bunge, wabunge hao hawataruhusiwa kuingia katika eneo la bunge hadi hapo watakapotimiza masharti waliyopewa.
Wabunge waliowekewa zuio hilo ni;
- Freeman Aikael Mbowe
- Ester Amos Bulaya
- Halima James Mdee
- John Wegesa Heche
- Joseph Osmund Mbilinyi
- Peter Simon Msigwa
- Rhoda Edward Kunchela
- Pascal Yohana Haonga
- Catherine Nyakao Ruge
- Devotha Mathew Minja
- Joyce John Mukya
- Aida Joseph Khenan
- Upendo Furaha Peneza
- Grace Sindato Kiwelu
- Joseph Leonard Haule.
Katika taarifa yake ya awali kuhusu wabunge hao kutohudhuria vikao vya bunge, spika aliwataka warejea Bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja, na kwa kuwa haijulikani walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya Virusi vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuingia Bungeni.
Wabunge hao walikoma kuhudhuria vikao vya bunge kwa maelezo kuwa wamejitenga na kujiweka chini ya uangalizi wakifuatilia mwenendo wa afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya virusi vya corona ama la.
Spika amesema wakati akiazimia hilo, tayari walikuwa wamelipwa posho za kujikimu kuanzia Mei 1 hadi Mei 17, 2020.