Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha 5 na vyuo vya ufundi 2019

0
43

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema wasichana wote waliofaulu katika mtihani wa kidato cha Nne katika mwaka uliopita wa 2018 wamefanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo mbali mbali vya ufundi nchini.

Jafo, ametoa kauli hiyo hii leo mjini Dodoma wakati akitangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka wa masomo utakao anza mapema mwezi Julai, 2019.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa wanafunzi, Jafo amesema wahitimu 110,331 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka 2019.

Amesema idadi hiyo ni kati ya watahiniwa 113,825 waliofaulu daraja la kwanza mpaka la tatu na kwamba wahitimu 108,644 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya elimu ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa Julai 8, 2019.

“Wanatakiwa kuripoti shuleni ndani ya siku 14 endapo atashindwa nafasi itachukuliwa na mwanafunzi aliyekosa nafasi,” amesema.

Amesema mabadiliko yoyote yataruhusiwa baada ya kukamilika kwa muhula wa kwanza wa masomo na zoezi hilo litazingatia uwepo wa nafasi katika shule kwa idhini wa ofisa elimu wa Mkoa.

Majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na vyuo vya ufundi

Send this to a friend