Makada wa CHADEMA waliohukumiwa jela maisha washinda rufaa

0
36

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imewachiwa huru makada wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya wizi, ubakaji na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Katala Kikaja na Ng’hulima Lilanga wameachiwa huru leo Novemba 16, 2022 baada ya uamuzi uliotolewa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Athuman Matuma kuridhika na hoja za warufani.

Kamanda aeleza mbinu zinazotumiwa na wanawake kuiba watoto Mwanza

Jaji Matuma amesema ushahidi uliowatia hatiani watu hao Aprili 12, mwaka huu ulikuwa dhaifu, unaotia mashaka na usiokubalika mbele ya macho ya sheria.

Makada hao  walitiwa hatiani kwa makosa mawili ya wizi, ubakaji, kuharibu mali na unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kukamatwa wakiwa kituo cha kupigia kura, Kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu walikokuwa mawakala wa wagombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020.

Send this to a friend