Makalla atangaza kuanza kwa mgao wa maji Dar es Salaam

0
44

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametangaza kuanza kwa mgao wa maji katika mkoa huo kutokana na upungufu wa maji katika vyanzo vya maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu ulikosababishwa na ukame.

Akizungumza leo Oktoba 25 baada ya kutembelea vyanzo vya vya kuzalisha maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu, Makalla amesema hali sio nzuri kwani kina cha maji cha vyanzo hivyo vyote kimepungua huku uzalishaji ukipungua kutoka lita za ujazo milioni 466 kwa siku hadi kufika lita milioni 300 sawa na asilimia 64 ya uzalishaji wote wa maji.

Kenya kuzalisha nishati ya nyuklia ifikapo 2038

“Naomba niwaambie wananchi kuwa mgao haupekuki kutokana na ukame ambao tayari TMA ilishatangaza kuwepo kwa hali hii muda mrefu kulikosabisha na kunyesha kwa mvua chache msimu wa mvua uliopita na kuchelewa kunyesha kwa mvua katika msimu huu wa vuli.

Pia watu waelewe hali hii haisababishwi na Serikali wala sera za CCM bali ni mipango ya Mungu, hivyo asitokee mtu huko akaanza kupotosha huko, kikubwa tuendelee kumuomba Mungu atuletee mvua za vuli na vyanzo vyetu vya maji viweze kujaa,” alisema Makalla.

Aidha, Makalla amesema jitihada nyingine ambazo serikali imezifanya kuanzia Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam, kamati zote za ulinzi na usalama zimewadhibiti watu wote ambao walikuwa wakichepusha maji na sasa kisingizo cha kuwa ni wao wanaosababisha uhaba wa maji hakipo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Dawasa, Cyprian Luhemeia alisema watatoa ratiba za mgao huo siku sio nyingi na kuwaomba wananchi kutumia vizuri maji yanayopatikana ili kuwafaa kwa nyakati hizi

Send this to a friend