Makamba aanza na TANESCO na EWURA

0
49

Waziri wa Nishati, January Makamba amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja (PBPA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA), kuhakikisha zinafanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya nchi na watanzania kwa jumla.

Amesema hayo wakati akizungumza na uongozi wa wizara hiyo pamoja taasisi zilizo chini yake, kwamba anahitaji kuona matokeo chanya katika utendaji kazi pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kusukuma mbele Sekta ya Nishati kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi na kukuza uchumi wa Taifa kwakuwa sekta hiyo ni muhimili muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Send this to a friend