Makamba: Tanzania ina gharama nafuu zaidi ya mafuta Afrika Mashariki

0
28

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Tanzania ndio nchi inayouza mafuta kwa gharama ndogo zaidi ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Ameyasema hayo alipotembelea Kijiji cha Kilando kata ya Kilando Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, katika ziara yake ya Kijiji kwa kijiji, lengo likiwa ni kukagua, kufatilia na kutatua kero za wananchi kwenye sekta ya nishati.

“Tumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, bila ruzuku ya bilioni 100 anayoitoa kila mwezi, bei ya mafuta ingekuwa imeongezeka shilingi 500 kwa kila lita ya dizeli na 200 kwa kila lita ya petroli,” amesema Waziri Makamba.

Bei ya mafuta nchini kwa upande wa petroli kwa sasa ni shilingi 3,220, huku bei ya dizeli ikiwa ni shilingi 3,143 kwa mujibu wa bei elekezi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Send this to a friend