Makampuni 19 ya Kimarekani kuangalia fursa za uwekezaji Tanzania

0
39

Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na Idara ya Huduma za Biashara ya Marekani umetangaza washiriki wa ziara ya siku mbili ya ujumbe wa Wafanyabiashara wa Kimarekani kutembelea Tanzania Bara na Zanzibar.

Ziara hiyo itafanyika kuanzia Agosti 27 hadi 28, 2022 ambapo makampuni 19 ya Kimarekani au yale yenye uwekezaji mkubwa nchini Marekani ambayo kwa pamoja yana uwekezaji wa zaidi ya Dola trilioni 1.6, yatatembelea miji ya Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na kuchunguza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania.

Ujumbe huo utakaoongozwa na Ubalozi wa Marekani kwa ushirikiano na matawi ya chama cha wafanyabiashara wa Kimarekani (American Chambers of Commerce – “AmCham”) katika nchi za Kenya, Tanzania na Afrika ya Kusini, utalenga kuzitambulisha kampuni za Kimarekani kuhusu fursa zilizopo katika masoko ya Tanzania na Zanzibar.

Mambo 6 yatakayobadilika baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa AmCham Kenya Maxwell Okello amesema “Wanachama wetu wana shauku kubwa kuhusu fursa mpya za kibiashara zinazofunguka Tanzania Bara na Zanzibar katika biashara za kilimo, nishati, huduma za afya, miundombinu, TEHAMA, uzalishaji viwandani na sekta nyingine za viwanda. Wanataka kulifahamu vyema soko hili na jinsi wanavyoweza kushiriki katika fursa hizi.”

“Ziara hii itawawezesha kupata taarifa muhimu na kuwasiliana moja kwa moja na wadau wanaohusika kutoka serikalini na sekta binafsi. Aidha, hii ni fursa muhimu kwa nchi zote mbili kujadili njia za kuimarisha zaidi uhusiano wa kibiashara baina yao ili kufikia malengo ya kiuchumi yanayosukumwa na uzalizaji mali na ongezeko la ajira.”ameongeza.

Makampuni hayo yataungana na wawakilishi kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Mjumbe wa Idara ya Huduma za Biashara ya Marekani katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Wizara ya Biashara ya Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara ya Marekani.

Send this to a friend