Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar azindua Mikopo ya Boti za Uvuvi ya NMB

0
13

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amezindua huduma ya mikopo nafuu ya boti za kisasa za uvuvi na vifaa vyake inayotolewa na Benki ya NMB, iitwayo ‘NMB MastaBoti’. Amemtaja Makamu wa Pili wa Rais kuwa msaidizi mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza Uchumi wa Buluu na kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.

Makamu wa Rais SMZ alisema hayo Jumanne, Januari 9, katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Tasini, iliyopo Kiwani Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar, wakati akizindua NMB MastaBoti. Wakati wa uzinduzi huo, boti tano pamoja na vifaa vyake vilivyokopeshwa na benki hiyo vilikabidhiwa kwa Jumuiya ya Wavuvi Kiwani (Juwaki).

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Makamu wa Pili wa Rais aliipongeza NMB kwa kusikiliza maombi ya Wana Kiwani na kuyafanyia kazi haraka. Alieleza kuwa boti hizo za kisasa zinaakisi na kusapoti dhamira na sera ya Uchumi wa Buluu inayotekelezwa na Serikali ya Zanzibar.

Aliwataka Juwaki kuhakikisha wanazitumia vizuri boti hizo na kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwapa fursa wengine. Pia, aliwahakikishia mafuta ya kuanzia kazi kwa boti zote. Aliomba NMB isaidie vifaa vya kuezekwa vyumba vya madarasa ya shule zilizoathiriwa na hali mbaya ya hewa, na kusaidia kununua mashine ya ultrasound kwa Hospitali ya Kiwani.

Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, alipongeza Serikali ya Zanzibar kwa mchakato wa Uchumi wa Buluu. Alisema ushirikiano wa karibu kati ya NMB na SMZ unategemea maono, mipango, na malengo ya serikali, na wamejitolea kuunga mkono malengo hayo.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiwemo Mawaziri na wabunge. NMB pia ilikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi kwa skuli tatu za Kiwani zenye thamani ya Sh. Milioni 22.

Send this to a friend