Makamu wa Rais Argentina ahukumiwa jela miaka sita

0
39

Makamu wa Rais wa Argentina, Cristina Fernández de Kirchner amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na kupigwa marufuku kuongoza ofisi ya umma baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya udanganyifu wa zaidi ya TZS trilion 2.33 inayohusiana na kazi za umma

Fernandez de Kirchner ambaye pia alikuwa Rais wa Argentina kwa mihula miwili kati ya 2007 na 2015 amepatikana na hatia Jumanne huku akiwa na zuio la kutotumikia kifungo hicho hadi rufaa yake itakapokamilika ambayo anatarajiwa kuifungua hivi karibuni kupinga hukumu hiyo.

Aidha, Wanasheria wamesema Fernandez hatakwenda jela hivi karibuni kutokana na uwezekano wa mchakato mrefu wa kukata rufaa ambao unaweza kuchukua hadi kipindi cha miaka mitatu pamoja na kinga yake alipokuwa makamu wa Rais.

Fernández amesema hukumu hiyo ni ya kisiasa na kutupia lawama mahakama kwa kushiriki katika ‘michezo michafu’.

Send this to a friend