Makamu wa Rais ataka utaratibu wa ufanyaji usafi mwisho wa wiki urudishwe

0
38

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema ni vema utaratibu wa kutumia siku za mwisho wa juma katika kufanya usafi wa pamoja kurudishwa ikiwemo katika maeneo ya barabara kuu ambayo yanakabiliwa na uchafuzi wa taka za plastiki kwa wingi.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na viongozi mbalimbali wa serikali wanaohusika na sekta ya mazingira nchini kilichofanyika mkoani Dodoma, amezitaka sekta hizo kujipanga upya na kuweka mikakati ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.

Aidha, ameagiza kuwekwa kwa utaratibu maalum wa ufuatiliaji wa uhifadhi wa taka katika usafiri wa umma ili kudhibiti uchafuzi unaofanywa na watoa huduma hiyo ya usafiri katika maeneo mbalimbali.

Katibu Mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Makamu wa Rais ameagiza wakuu wa mikoa kusimamia zoezi la kusafisha mitaro ikiwa ni njia ya kuimarisha usafi wa mazingira pamoja na kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Nino zilizotabiriwa.

Halikadhalika, amesisitiza elimu kwa wananchi kuendelea kutolewa kuhusu uhifadhi wa mazingira pamoja na kudhibiti uandaaji mashamba kwa kuchoma moto bila tahadhari hali inayopelekea athari kubwa kwa binadamu,viumbe hai na mazingira.

Send this to a friend