Makarani 10 wapoteza maisha katika kipindi cha Sensa

0
38

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022, Anne Makinda amesema katika zoezi la Sensa mwaka huu jumla ya Makarani 10 wamepoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiua na kuuawa.

Makinda ametoa taarifa hiyo akiwa mkoani Manyara wakati alipokutana na Kamati ya Sensa Mkoa wa Manyara kwa lengo kupokea taarifa ya zoezi la Sensa.

“Mmoja wa Tabora alijinyonga mwenyewe na kuacha ujumbe, wengine walikufa kwa maradhi na mwingine aliuawa baada ya kupata vijisenti kidogo wenzie wakadhani ana mamilioni,” ameeleza Makinda.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema Mkoa wa Manyara umefanikiwa kukamilisha zoezi la Sensa ambapo wamezifikia zaidi ya Kaya 300,000 ikiwa ni sawa na asilimia 126 ya lengo.

Send this to a friend