Makarani waonywa kwenda na vishkwambi sehemu za starehe

0
46

Siku chache baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuanza Agosti 23, 2022, Serikali imewaonya makarani wa Sensa kuacha tabia ya kwenda sehemu za starehe na vishkwambi ili kuepuka kuibiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa madai ya kuwepo kwa wizi wa vifaa hivyo hasa katika mikoa ya Njombe, Arusha na Simiyu.

Karani ajiua saa chache kabla ya Sensa, aacha ujumbe

Amewataka makarani mara baada ya kumaliza kazi zao jioni, wahakikishe wanapeleka vifaa hivyo nyumbani kwanza kwakuwa ndio mahali salama kisha waende sehemu za starehe.

Aidha amebainisha kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kuvinunua vishkwambi, hivyo vifaa hivyo vinapoibiwa huisababishia hasara kubwa Serikali.

“Niwaombe wananchi wenye lengo la kuviiba vishkwambi ambavyo hutumika kwa kuandika taarifa za wananchi katika kazi ya sensa kuacha kwa kuwa siyo busara kuiba kifaa ambacho kinatumika kukuhesabu wewe mwenyewe,” amesema.

Send this to a friend