Makardinali kuamua tarehe ya mazishi ya Papa Francis leo

0
4

Makardinali wanatarajiwa kukutana siku ya leo ili kuamua tarehe ya mazishi ya Papa Francis, aliyefariki dunia siku ya Jumatatu nyumbani kwake Vatican, akiwa na umri wa miaka 88.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki amefariki baada ya kupatwa na kiharusi kilichosababisha moyo wake kushindwa kufanya kazi kabisa.

Kwa mujibu wa Katiba ya Kitume, mazishi ya Papa yanapaswa kufanyika kati ya siku ya nne hadi ya sita baada ya kifo chake. Hata hivyo, maamuzi ya mwisho yatafanywa na makardinali.

Viongozi wa nchi na familia za kifalme wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Papa Francis yatakayofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro (St Peter’s Basilica), ambapo Rais wa Marekani, Donald Trump, amekuwa wa kwanza kutangaza kuhudhuria.

Send this to a friend