Makonda aagiza barabara itengwe kwa ajili ya maonesho ya biashara kwa wajasiriamali

0
49

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa kutenga barabara maalumu katikati ya jiji hilo ili itumike kwa ajili ya maonesho ya kibiashara kwa wajasiriamali kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi na kamati mbalimbali za maandalizi ya sherehe za wafanyakazi ambapo ameelekeza kuwa barabara husika iwe kwa ajili ya wafanyabiasha wa mavazi ya asili, picha, vinyago na bidhaa nyingine za urembo na mapambo.

Makonda amesema wananchi wa Mkoa huo wanapaswa kunufaika na shughuli mbalimbali za kitaifa zinazofanyika mkoani hapo, hivyo kuwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa zinazotokana na ugeni ambao tayari umeshaanza kuwasili ili kujiandaa na sherehe hizo.

Aidha, Makonda amewahakikishia usalama wa kutosha wakazi wa Arusha na wageni wote wanaofika mkoani Arusha kwenye shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Mei Mosi.

Send this to a friend