Makonda aagiza mawaziri kuandika ripoti za utendaji kazi wao

0
17

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amewaagiza mawaziri wote nchini kuandaa taarifa katika kila robo ya mwaka wa bajeti na kuiwasilisha kwenye sekretarieti ya chama Taifa inayoelezea utekelezaji wa kazi waliyopewa na Serikali ili kujua utendaji wao wa kazi.

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya mapokezi, amesema waziri yeyote ambaye hatawasilisha ripoti yake inayoonesha utekelezaji wa ilani, Chama cha Mapinduzi hakitasita kumchukulia hatua.

“Waziri yeyote ambaye atakaa ndani ya robo ya mwaka hajafanya kazi, hana ripoti, hakuna utekelezaji wa ilani, chama hakitasita kumchukulia hatua kwani hivi sasa ni wakati wa kufunga mkanda kuwatumikia wananchi,” amesema.

TCAA yafafanua kuhusu kibali cha helikopta ya CHADEMA

Aidha, amewataka makatibu wote wa CCC nchi nzima kutoa taarifa ya viongozi wa Serikali wanaokwenda kwenye mikoa kufanya ziara bila kuripoti kwenye ofisi za chama.

“Imekuwepo kasumba ya viongozi wanaofanya ziara hawaendi kwenye ofisi za katibu wa mkoa, hawaendi kwenye ofisi za katibu wa wilaya, chama kinashituka tu watu wako mitaani [..] kila waziri na naibu Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya anaowajibu wa kuripoti kwenye ofisi za chama na kueleza anakwenda kufanya nini,” ameeleza.

Send this to a friend