Makonda na Lemutuz washtakiwa kwa tuhuma za kupora Range Rover

0
55

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na William Malecela maarufu Lemutuz wamefunguliwa kesi mahakamani kwa tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover.

Makonda na Lemutuz wamefunguliwa kesi hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelwe ambaye katika madai yake anataka alipwe fidia ya zaidi ya TZS milioni 240 ambazo ni gharama za kodi na thamani ya gari hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Wakili wa mfanyabiashara huyo, Kung’e Wabeya amesema tayari mahakama hiyo imetoa taarifa kwa wadaiwa kuhusu kesi hiyo na kuwataka wawasilishe mahakamani utetezi wao wa maandishi ndani ya siku 21 tangu kupokea taarifa hiyo.

TRA kutaifisha magari yenye namba zisizotambulika

Ameongeza kuwa endapo wadaiwa watashindwa kuwasilisha mahakamani utetezi wao ndani ya muda huo, mahakama itaweza kutoa hukumu dhidi yao.

Wabeya amesema kesi hiyo ya madai namba 234 ya mwaka 2022 imepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Oktoba 13, 2022 saa 7 mchana.

Send this to a friend