Makosa 6 ya kuepuka unapoamka asubuhi

0
44

1.Kuangalia simu mara unapoamka
Unapoanza siku kwa kuangalia simu yako, unatamani kuangalia ulichokikosa. Pia, siku yako huanza kama kulinganisha na maisha ya watu wengine, inaweza kukunyong’onyesha, na kupunguza ari ya akili yako mpya ambayo ingeweza kutumika vinginevyo kutimiza mambo yenye matunda.

2.Kuahirisha kuamka
Watu wengi hupenda kusinzia mara mbili au tatu kabla ya kuamka. Weka kengele kwa wakati unaotaka kuamka, mara kengele inapolia, zima na uondoke kitandani. Utafiti mmoja wa mwaka 2018 ulibainisha kuwa kugawanyika kwa usingizi kunaongeza usingizi wa mchana na kupungua kwa utendaji.

Pia, haishangazi kwamba tunahisi hali isiyo ya kawaida kiakili na kimwili tunapolazimika kuamka dakika 10 baadaye.

3.Kuamka kwa ghafla
Upe mwili wako muda wa kutosha wa kukabiliana na kuamka. Jinsi mwili na akili yako inavyofanya kazi wakati umelala ni tofauti na unapokuwa macho,  mwili wako unahitaji dakika chache kujiandaa kwa hali ya kuamka. Usitumie muda mrefu, dakika moja kitandani inatosha kwa mwili kuzoea.

4.Kuruka kifungua kinywa
Kuruka kifungua kinywa kunaweza kusababisha viwango vya chini vya nishati sababu tumbo lako linakuwa tupu tangu ulipokula chakula cha jioni. Pia, huongeza uwezekano wa kula chakula kingi cha mchana kwa sababu ya njaa ya muda mrefu. Hivyo, hakikisha unapata kifungua kinywa kitakachokupa nguvu na afya.

5.Kutokunywa maji
Vivyo hivyo kwa maji, mwili wako unanyimwa maji tangu ulipolala. Imarisha mwili wako baada ya kuamka ili mwili ufanye kazi vizuri.  Glasi moja au mbili za maji  husaidia kujaza hifadhi za maji mwilini mwako.

6.Kuepuka mazoezi
Kuchagua kufanya mazoezi asubuhi kunaweza kuwa na manufaa kwa kuongeza viwango vyako vya nishati siku nzima. Kipindi cha kukimbia haraka asubuhi au kunyanyua miguu kinaweza kukusaidia kuhakikisha kuwa unaanza siku yako na hali bora zaidi.

Kwa kuvunja baadhi ya tabia hizi mbaya, unaweza kuhakikisha kwamba mchakato wa shughuli yako ya kila siku unaweza kuimarishwa.