Makundi 47 ambayo RC Ally Hapi ameyataka yawe na vitambulisho vya wajasiriamali

0
28

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesitisha likizo za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zilizomo mkoani humo kufuatia mkoa huo kufanya vibaya katika ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Mbali na kufuta likizo zao, Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri RC Hapi aliwataka watumishi hao kutosafiri nje ya Mkoa huo baada ya huku kuwapa muda wa wiki tatu kuhakikisha wafanyabiashara wote wanapata vitambulisho hivyo.

Amebainisha kuwa, lengo la Rais John Magufuli aliyegawa vitambulisho hivyo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini ni kutaka wafanyabiashara wanatambuliwa na kuchangia maendeleo ya nchi kwa kulipa kodi.

Amewaonya watendaji wa vijiji na Serikali wanaodai kuwa vitambulisho vinasababisha mapato kupungua, akidai kuwa hiyo ni hoja dhaifu.

Hapi ameanisha makundi zaidi ya 40 ambayo yanastahili kupata vitambulisho hivyo, wakiwemo waandishi wa habari, wapiga debe, wauza mahindi, mchicha, Waganga wote wa Tiba za jadi, wanachama wote wa vikundi vya vikoba, vilabu vyote vya pombe za kienyeji.

Amesema hakujiandaa kushindwa katika ugawaji wa vitambulisho na ndio sababu ya kusitisha likizo za viongozi hao ili wagawe vitambulisho hivyo ndani ya muda aliouweka ili Mkoa huo uweze kushika nafasi ya tatu katika ugawaji huo.

Kwa mujibu wa Hapi, Mkoa huo ni wa tano kutoka mwisho katika ugawaji huo wa vitambulisho. Ametoa hadi tarehe 17/06/2019 makundi hayo yawe tayari yamegawiwa vitambulisho.

Makundi hayo ni pamoja na:

  1. Vibarua wa viwandani wasio na mikataba maalum.
  2. Wafanyakazi wote wanaofanya kazi kwa wenye maduka/stoo za jumla.
  3. Wabeba mizigo wote kwenye stendi zetu.
  4. Wafanyakazi kwa wamama/baba ntilie.
  5. Wachuuzi kwenye mialo yote.
  6. Vibarua wote wa viwanda/mashine za kusaga unga au kukamua mafuta ya Alizeti.
  7. Wafanyakazi wote walio kwenye saloon za aina zote.
  8. Wale wote wanaopeleka kuuza chai kwenye viwanda vya chai toka mashamba binafsi.
  9. Wafugaji biashara wote wa Ng’ombe na kuku.
  10. Vibarua kwenye garage zote.
  11. Wachomeleaji (welder) wote.
  12. Vibarua wote kwenye karakana za Uselemala.
  13. Vibarua wote kwenye vijiwe vya nyama choma/chips.
  14. Wapiga debe wote kwenye stend za Iringa.
  15. Wanachama walio kwenye vikundi vyote vilivyopewa Mikopo.
  16. Vibarua wote walio kwenye Migodi yetu.
  17. Wanachama wote wa Saccos za Iringa.
  18. Vibarua wote kwenye vibanda vya simu.
  19. Wafanyakazi wote kwenye Supermarket
  20. Wafanyakazi wa vituo vya Mafuta.
  21. Vibarua wote katika Mashamba ya miti.
  22. Wanaochoma mahindi barabarani, ya kutafuna.
  23. Wafanyakazi wa guest wote
  24. Wafanyakazi wa restaurants wote.
  25. Wafanyakazi wote wa baa.
  26. Waliowezeshwa na Mfuko wa Tasafu na waliopiga hatua kwa msaada huo.
  27. Wanaolima na kuuza kibiashara bustani za mboga.
  28. Waganga wote wa Tiba za jadi.
  29. Wanachama wote wa Vikundi vya vikoba.
  30. Vilabu vyote vya pombe za kienyeji.
  31. Madereva wote wa daladala, bodaboda, mabasi, Hiace.
  32. Makondactor wote wasio na Mikataba rasmi.
  33. Wajasiliamali wote kandokando mwa barabara.
  34. Wafanyakazi wote katika Butcher za nyama/samaki.
  35. Wafanyakazi wote wa carwash.
  36. Waandishi wa habari wote.
  37. Wanaofyatua tofali za biashara wote.
  38. Walio kwenye sector ya Utalii wote.
  39. Vibarua kwa wakandarasi wote na mafundi wote wa nyumba.
  40. Wafugaji wa nyuki wote.
  41. MCs wote na wapiga picha.
  42. Madalali wote wa nguzo, nyumba, mashamba, mazao nk.
  43. Wakusanya mazao wote.
  44. Wanaokopi/rekodi nyimbo Vibarazani mwa maduka.
  45. Freelenser wote wa makampuni wa simu.
  46. Wauzaji wote wa rejareja wa vitenge, nguo, matunda, chukula wanaopita maofisini.
  47. Walinzi wote walioajiriwa na watu/taasisi wasiokuwa na mikataba rasmi.
Send this to a friend